Mapenzi ni kitu kizuri sana kama upo kwenye mahusiano sahihi na mapenzi ni
kitu kibaya sana kama utakuwa kwenye mahusiano yasiyo sahihi. Umewahi kujiuliza
ni kwa nini uliyenaye anakupenda sana na umewahi kupata majibu ya hayo
maswali!!??
Kama umewahi kujiuliza na kupata majibu basi ni vizuri sana kwa upande wako
na kama umewahi kumuuliza hata yeye na akakupa majibu pia ni vizuri ingawa huwa
inakuwa vigumu sana mtu kukupa sababu zote kwa nini anakupenda.
Ukiachilia mbali sababu zinginezo BINAFSI za mtu kukupenda lakini pia hizi
zifuatazo ni baadhi ya sababu za kawaida tu ambazo mtu anayekupenda huwa anazo.
1.
UNAMJALI
Hakuna kitu kizuri kama kujaliwa na unayempenda na
ndio kitu muhimu sana kwenye mapenzi. Ukionyesha kujali kwenye mapenzi basi
hata vitu vingine vingi huenda kwenye mstari ulio salama na hufanya mapenzi
yenu kuwa nyoofu siku hadi siku.
2.
UNAMSAIDIA
Hiki pia ni kitu bora sana kwenye mapenzi hasa kwa
kutambua kuwa mojawapo ya njia nzuri za kudumisha mapenzi ni pamoja na
kusaidiana pale linapotokea tatizo lolote lile kwa mmojawapo kati yenu. Jitolee
kwa kila khali kwa mpenzi wako pale anapopata shida/tatizo lolote.
3.
UNAMRIDHISHA
Yeah ni kitu safi sana kuwepo kwenye mahusiano
ambayo kila mtu anaridhika na mwenzake. Iwe ni kwenye mambo ya kawaida au hata
yale mambo ya ndani. Ukiridhika na huyo uliyenaye na ukaridhika kwa kila
anachokupa basi mapenzi huenda murua kabisa.
4.
UNAMTETEA
Unapoonyesha kuwa upande wa mwenzi wako kwenye kila
tatizo au challenge yoyote inayotokea basi huwa ni njia nzuri sana nay a msingi
kudumisha mapenzi yenu. Kuna mengi yanatokea kila siku kwenu ila jitahidi kila
mara kumtetea kwa lolote mbele yake isipokuwa tu labda liwe kweli amekosea na
hapo mrekebishe katika hali ya kimapenzi zaidi bila kumkwaza.
5.
MVUMILIVU/HUNA TAMAA
Hii ni kitu njema sana nay a busara sana kwenye
mapenzi na hupendwa hasa na sie wanaume pale linapokuja suala la mahusiano ambapo
huwa tunapenda sana wanawake wasio na tamaa na ni wavumilivu kwa lolote ndani
ya mapenzi. Hatupendi wasichana wanaoshoboka kwa vitu vidogo na vya muda na
kuishia kuharibu mapenzi.
6.
UNAMPA CHANGAMOTO/CHALLENGES
Unapokuwa kwenye mahusiano haina maana basi kila
anachofanya mpenzi wako ni sahihi hata kama unaona anakosea. Kama unaona hayupo
kwenye njia sahihi basi mpe ushauri/changamoto ili aweze kubadilika na sio kila
kitu kuwa mtu wa kumuitikia ‘’NDIO’’ tu kitu ambacho hakijengi bali kinabomoa.
7.
MKWELI
Hii pia ni changamoto mojawapo kwenye mapenzi hasa
pale unapokuwa kwenye mapenzi na mtu na mkawa mna ndoto za kufika mbali, kuwa
mkweli ni kitu kizuri sana kwa mpenzi wako kwani huweza kukuondolea vikwazo
vingi na kutokuwa na wasiwasi kwa kila kitu kwenye mahusiano yenu.
8.
UNA MSIMAMO
Msimamo thabiti hujenga mapenzi imara na yaliyo
bora sana. Usipokuwa na msimamo kwenye mapenzi basi husababisha mapenzi/mahusiano
yenu kuyumba mara kwa mara na mwishowe kuvurugika kabisa na kuisha mara moja. Jenga
tabia ya kuwa na msimamo ili usiyumbe wewe wala mpenzi wako.
9.
UNAJIAMINI
Hii pia ni mojawapo ya kitu safi sana kwenye
mapenzi na inayoweza kumfanya mpenzi wako kukupenda zaidi kwa kujiamini kwako
katika kila kitu na kutokuwa na hali ya uoga wala kuchanganywa na vitu vidogo
nje au ndani ya mahusiano. Jenga tabia ya kujiamini ikusaidie kwenye maisha
yako binafsi na hata ya mahusiano.
10. UNAMUOGOPA
MUNGU
Ukiwa na tabia njema na maadili mema basi hata
mahusino yako yatakuwa mema kwani utamtanguliza Mungu katika kila jambo na
utakuwa mfano bora kwa mpenzi wako na kumfanya akupende na kukuchukulia kama
role model wake linapokuja suala la imani na kumpenda Mungu. Jenga tabia ya
kutenga muda Fulani wewe na mwenzi wako ili kujiweka mbele za Mungu na kusali
ili msiyumbe kwenye maisha na ili kuweza kusonga mbele katika lolote kwa nguvu
zake yeye pekee.
NB; Nia hasa ya kuandika hizi sababu ni kuwa kama ulikuwa either umejisahau
au katika haya hukuwa unamfanyia mpenzi wako kimojawapo basi anza sasa
kumfanyia ili kuweza kuimarisha zaidi mahusiano yenu.




No comments:
Post a Comment